Jengeni mawazo bora pamoja kwenye Google Docs
Tayarisha na ushirikiane kwenye hati za mtandaoni katika muda halisi na kwa kutumia kifaa chochote.
Urahisi wa kushirikiana, popote pale
Badilisheni hati pamoja katika muda halisi mkiwa na uwezo wa kuzishiriki kwa urahisi na mtumie vipengele vya maoni, mapendekezo na majukumu ili mwendeleze mambo yenu. Mnaweza pia kutumia kipengele cha kutaja kwa @ kushirikisha watu, faili au matukio yafaayo kwenye Hati zenu za mtandaoni ili kuboresha ushirikiano.
Andika haraka ukitumia umahiri ulio ndani ya programu
Vipengele saidizi kama vile vya Utungaji Mahiri hukusaidia kuandika haraka na kupunguza makosa ili umakinikie mawazo yenyewe. Okoa muda pia kwa kutumia vipengele vya mapendekezo ya tahajia na sarufi, kuandika kwa kutamka na kutafsiri hati haraka.
Unganisha programu zako nyingine za Google kwa urahisi
Kwa manufaa yako, Google Docs imeunganishwa na programu nyingine za Google unazozipenda, kwa hivyo inakuokolea muda. Jibu maoni moja kwa moja kutoka Gmail, pachika chati kutoka Google Sheets na ushiriki kupitia Google Meet kwa urahisi. Unaweza hata kutafuta kwenye wavuti na Hifadhi ya Google ili upate maudhui na picha zinazokufaa moja kwa moja kwenye Google Docs.
Leta ushirikiano na umahiri kwenye aina nyingine za faili
Badilisha faili za Microsoft Word mtandaoni kwa urahisi bila kuzigeuza na ujazilie vipengele vya kina yva Google Docs ambavyo ni vya kushirikiana na vya usaidizi kama vile majukumu na Utangaji Mahiri. Unaweza pia kuleta PDF na papo hapo zitaweza kubadilishwa.
Fanya mengi zaidi kwa kutumia programu jalizi
Fikia programu mbalimbali za wengine, moja kwa moja kwenye Hati za Google. Iwe ni programu ya kutia sahihi pepe au zana ya usimamizi wa miradi, ifungue kwenye Hati za Google ili ufanye kazi haraka.
Shughulikia maudhui mapya
Kwa kutumia Hati za Google, kila mtu hufanya kazi kwenye nakala mpya zaidi ya hati. Kwa sababu mabadiliko yoyote unayoyafanya huhifadhiwa kwenye historia ya nakala, ni rahisi kufuatilia au kutendua mabadiliko.
Dumisha tija yako, hata ukiwa nje ya mtandao
Unaweza kufikia, kuunda na kubadilisha Hati za Google hata bila muunganisho wa intaneti, hii inakusaidia kuongeza tija ukiwa mahali popote.
Usalama, utiifu na faragha
Ni salama kwa chaguomsingi
Tunatumia hatua za usalama ambazo ni bora zaidi katika sekta hii ili kuweka data yako salama, ikiwa ni pamoja na ulinzi wa kina dhidi ya programu hasidi. Hati za Google zimeundwa mahususi kutumika kwenye wingu, kwa hivyo hakuna haja ya kuweka faili kwenye kifaa na hivyo hupunguza hatari kwa vifaa vyako.
Usimbaji fiche wakati wa kupitisha na usio wa kupitisha
Faili zote zilizopakiwa kwenye Hifadhi ya Google au zilizoundwa kwenye Hati za Google husimbwa kwa njia fiche wakati zinapitishwa na wakati hazipitishwi.
Utiifu unaotuwezesha kutimiza matakwa ya sheria
Bidhaa zetu, ikiwa ni pamoja na Hati za Google, mara kwa mara hupitia uthibitishaji huru wa usalama, faragha na vidhibiti vya utiifu.
Huduma iliyoundwa kwa kuzingatia faragha
Hati za Google hufuata ahadi madhubuti za faragha na ulinzi wa data, sawa na huduma zingine za Google Cloud kwa biashara.
Unadhibiti data yako.
Hatutumii kamwe maudhui yako ya Hati za Google kwa madhumuni ya utangazaji.
Hatuuzi kamwe taarifa zako binafsi kwa wahusika wengine.
Tafuta mpango unaokufaa
Hati za Google ni sehemu ya Google Workspace
Kila mpango unajumuisha
Kwa Matumizi Binafsi (Bila malipo) |
Business Standard$12 USD
kwa kila mtumiaji kwa mwezi, ahadi ya mwaka 1 Au $14.40 kwa kila mtumiaji kwa mwezi, unapolipia kwa kila mwezi
|
|
|---|---|---|
|
Hati, Majedwali, Slaidi, Fomu za Google
kubuni maudhui |
||
|
Hifadhi ya Google
Hifadhi salama ya wingu |
GB 15 kwa kila mtumiaji |
TB 2 kwa kila mtumiaji |
|
Hifadhi za pamoja za timu yako |
||
|
Gmail
Barua pepe salama |
||
|
Anwani maalum ya barua pepe ya biashara |
||
|
Meet
Kufanya mikutano ya video na ya sauti |
Washiriki 100 |
Washiriki 150 |
|
Rekodi za mikutano huhifadhiwa kwenye Hifadhi ya Google |
||
|
Msimamizi
Usimamizi chini ya mamlaka moja |
||
|
Vidhibiti vya sera za usalama kulingana na kikundi |
||
|
Usaidizi kwa wateja |
Usaidizi wa kujihudumia mtandaoni na majadiliano ya jumuiya |
Usaidizi mtandaoni usiku na mchana, kila siku na majadiliano ya jumuiya |
Shirikianeni mkiwa popote pale, kwenye kifaa chochote
Fikia, tayarisha na ubadilishe hati zako mahali popote ulipo — kwenye kifaaa cha mkononi, kompyuta kibao au kompyuta — hata ukiwa nje ya mtandao.
Piga hatua kwa kutumia violezo
Chagua kwenye violezo mbalimbali vya dashibodi, hati za kufuatilia miradi na violezo vingine vilivyounda kitaalamu ili uanze kufanya mambo haraka.
Tembelea Matunzio ya Violezo vya Hati za Google kwa maelezo zaidi.